SpotifyToMP3
Ambwene Mwasongwe-Hatatuacha

Ambwene Mwasongwe-Hatatuacha

9:15 · 87,723 plays

From the album Ambwene Mwasongwe

Description

Hatatuacha ni wimbo wa kufariji na kutia moyo watu wanaopitia changamoto nyingi za maisha, hasa baada ya kupoteza matumaini kwa sababu ya kupoteza watu waliowategemea na watu muhimu katika maisha yao. Wimbo huu ni habari ya kweli ya mabinti wawili ambao walinikuta studio Mwaka 2010 wakati naandaa Albamu ya Misuli ya Imani. Waliposikia shuhuda za nyimbo kadhaa nilizoimba walitiwa moyo na wakaamua kunisimulia mkasa wa maisha yao, maana walikuwa wamepoteza baba yao huku wakibaki na mama yao ambaye maisha yake yalikuwa magumu. ushuhuda wao ulinigusa na nikapata kunukuu baadhi ya maneno toka kitabu cha Maombolezo sura ya 5 na baadhi ya maneno ya Zaburi Sura ya 68 na maneno hayo yaliwatia moyo na wakasimama na kwa sasa wamefanikiwa na Mungu aliwakumbuka na wanaendelea mbele. Nimeamua kuachia huu wimbo Mwaka huu baada ya kuguswa na kuongozwa na Roho Mtakatifu kuwatia moyo wote wanaopitia magumu ningependa kuwaimbia na kuwaambia WASIOGOPE MUNGU HATATUACHA. Wimbo huu ukakuinue nawewe tena na ukafanikiwe katika mambo yako na hata kama unalia leo lakini ushindi uko mbele..... kumbuka HATATUACHA.

You May Also Like